Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imefanikiwa kufuzu hatua ya raundi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 5-0 dhidi ya wapinzani wao.
Katika mchezo wa marudiano uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Yanga walithibitisha ubora wao kwa ushindi wa mabao 2-0, huku magoli yakifungwa na Pacome Zouzoua pamoja na Aziz Andabwile.
Ushindi huu umeongeza nguvu kwa kikosi cha Yanga, ambacho katika mchezo wa kwanza kiliibuka kidedea kwa mabao 3-0, na hivyo kuhitimisha jumla ya mabao 5-0 katika hatua hii.
Kwa matokeo haya, Yanga wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, huku wakitarajiwa kukutana na wapinzani wenye kiwango cha juu zaidi katika raundi inayofuata.

0 Comments