Usiri umegubika kikao maalum cha kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA),kinachoendelea katika Hoteli ya Golden Tulip,Masaki ,Jijini Dar es salaam.
Inaelezwa kuwa miongoni mwa agenda wanazojadili mbali ya maandalizi ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho,ni kujadili majina ya walioomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Kikao hicho kilichoanza leo mchana, kinatrajwa kuwa ni cha hatua ya mwisho ya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chaumma,utakaofanyika kesho Agosti 7,2025 katika ukumbi wa Mlimani city.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na viongozi wa ndani wa Chama hicho,vikao vya leo vinapokea na kujadili majina hayo ya watiania, mbele ya Halmashauri Kuu kwa ajili ya kuchujwa na kujadiliwa kujadiliwa kwa kina kabla ya kupitishwa rasmi kesho kwenye Mkutano Mkuu.
Hili ni tukio muhimu sana kwa chama chetu,kikao hiki kinaangalia kwa undani sifa na uwezo wa kila mmoja aliyejitokeza,tukilenga kumpa mgombea bora mwenye dira na maono ya kweli kwa Taifa amesema msemaji wa chama hicho John Mrema.
Amesema kikao hichi kinaongozwa na kiongozi wa kitaifa Hashimu Rungwe ambaye ameshiriki mara tatu katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
.jpg)
0 Comments