Header Ads Widget

JOB NDUGAI AFARIKI DUNIA


Aliye wahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai,amefariki Dunia jijini Dodoma,taarifa ya Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson,aliyeitoa Jumatano,Agosti 6,2025 imesema kifo cha Ndugai kimetokea hii leo jijini Dodoma.Sababu ya kifo chake haijaeleweka.

Mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Kwa masikitiko makubwa naomba taarifa ya kifo cha kiongozi wetu,mwanasiasa mkongwe na spika Mtaafu Mheshimiwa Job Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya Marehemu ndugu jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa,Mwezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi kigumu alisema Tulia.

Ndugai kabla ya kifo chake aliibuka mshindi katika kura za maoni,kuwania ubunge katika jimbo la kongwa mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania,zilizopigwa hivi karibuni.

Ndugai alihudumu katika nafasi ya Spika wa Bunge kwa miaka 6 kuanzia mwishoni mwa 2015 hadi alipojiuzulu Januari 2022.

Pamoja na kuwa mahiri kwa kuzifahamu vyema kanuni za Bunge,aliwahi kukosolewa kwa kutoa kauli tata ikiwemo kusema alikuwa na uwezo wa kumzuia mbunge yeyote asinzungumze kabisa bungeni.

Pia aliwahi kukosolewa kwa kusema aliyekuwa Rais wa awamu ya tano,John Magufuli angelazimishwa kuendelea kugombea urais baada ya kumaliza vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba atake asitake



 

Post a Comment

0 Comments