ACT Wazalendo imemuidhinisha rasmi bwana Luhaga Mpina kuwa mmoja wa wagombea wa Urais atakayechuana na Rais Samia Suluhu Hassan wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Uamuzi huo umefikiwa na Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo jijini Dar es salaa, ambaye ilipendekeza majina mawili,Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.
Majian hayo yaliyopendekezwa yaliwasilishwa kwa Mkutano Mkuu Taifa kwa ajili ya kupigiwa kura,ambapo katika mkutano huo,Mpina alichaguliwa kwa kishindo kwa kupata kura 559 sawa na asilimia 92.3 ya kura zote 610 zilizopigwa.
Luhaga Mpina amemshinda Mgombea mwenzake Kalikawe ayepata kura 46 sawa na asilimia 7.7 na sasa Mpina atapeperusha bendera ya ACT katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025,mgombea mwenza akiwa Bi. Fatma Ferej
Kwa upande wa Zanzibar,Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Othuman Masoud Othuman amechaguliwa kuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupata kura 606 za ndio sawa na asilimia 99.5 ya kura zote halali 609.
.jpg)
0 Comments