Mwenyeji Tanzania wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024,baada ya kuibuka na ushindi mwembamaba wa bao 1-0 dhidi ya Mauritania, bao lililopatika dakika za lala salama na beki fundi wa mpira Shomari Kapombe.
Mchezo huo wa kundi B ulifanyika Jumatatu usiku katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam,ambapo mashabiki walishuhudia dakika 88 za mvutano kabla ya Kapombe kufunga bao hilo muhimu,akimalizia pasi ya kiufundi sana kutoka kwa Iddy Nado na kumtungua kipa wa Mauritania Abderrahmane Sarr,na kuzua shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.
Ushindi huo unakuwa wa pili kwa Taifa stars katika mechi mbili za mwanzo, na sasa wanaongoza kundi B kwa alama sita bila kuruhusu bao lolote hatua inayowaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu hatua ya mtoanao.
.jpg)
0 Comments