Header Ads Widget

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU TANZANIA ZAANZA RASMI LEO,VYAMA VYAJIANDAA KWA MSHIKE MSHIKE


Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania Bara na Visiwani kwa mwaka huu 2025,zimeanza rasmi leo,kwa mujibu wa ratiba ya INEC.

Hata hivyo,uchaguzi huu unatarajiwa kutokuwa na hamasa ya mshikemshike baada ya chama kikuu cha upinzani kutangaza kutoshiriki,kikidai mfumo wa uchaguzi wa sasa unakinufaisha chama tawala na hautoi usawa wa ushindani.

Kwa majibu ya INEC, jumla ya vyama 18 vilivyosajiliwa vitashiriki uchaguzi huu,vikiwa na wagombea 17 wa urais.

Hali hiyo inatokana na mgombea wa urais wa ACT, Luhaga Mpina kutoidhinishwa na INEC baada ya kubaini uteuzi wake ulikuwa kinyume na taratibu za kikatiba na haukufata sheria za chama.

Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa pia ilimwengua rasmi kufuatia pingamizi lililotolewa na mwanachama wa chama hicho,Monalisa Ndala sababu kuu iliyoelezwa ni kwamba Mpina alipata uanachama wa ACT mnamo Agosti 5,2025 nje ya muda wa kisheria kwa kuchukua fomu za kugombea ndani ya chama,amabo ulipaswa kuwa kabla ya Mei 25,2025.

Hali hii imepelekea chama cha ACT kutoshiriki nafasi ya urais mwaka huu.

Hata hivyo ACT imepeleka shauri lake Mahakamani kupinga uamuzi wa Msajili na INEC, CCM kimepanga kuzindua rasmi kampeni au hekaheka zake kulekea uchaguzi mkuu leo Agosti 28,2025 katika Viwanja vya Tanganyika Packers,Kawe Dar es salaam,Mwenyekiti wa CCM na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hssan,Ataongoza uzinduzi huo akifuatana na mgombea mwenza wake Dkt Emmanuel Nchimbi.

Uzinduzi huo utaashiria mwanzo mzuri wa kampeni za urais,ubunge na udiwani nchi nzima,huku chama hicho kitakuwa cha kwanza kufanya uzinduzi wa kampeni za mwaka huu, kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29.2025.

 

Post a Comment

0 Comments