Header Ads Widget

KESI YA TUNDU LISSU YAPIGWA MARUFUKU KURUSHWA MBASHARA


Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu,jijini Dar es salaam,imepiga marufuku kurushwa mubashara kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Lissu,katika hatua ya kusomewa maelekezo ya mashahidi.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Franco Kiswaga,baada ya kukubaliana na ombi la upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga,uliolenga kulinda uasalama na utambulisho wa mashahidi.

Hakimu alisema kuwa hatua hiyo haiwazuii wananchi wala mshtakiwa kusikiliza kesi hiyo bali inalenga kuzuia kufichuliwa kwa mashahidi wa siri.

Kuzuia kurushwa mubashara hakumzuii mashtakiwa kusikiliza bali kuna zuia ueneaji unaoweza kuhatarisha wa mashahidi alisema Hakimu.Kwa mujibu wa amri hiyo nyombo vya habari au watu binafsi wamekatazwa kuchapisha au kusambaza nyaraka zozote zinazoweza kufichua majina anuani au taarifa binafsi za mashahidi isipokuwa kwa ruhusa ya Mahakama.

Uamuzi huu unafuatia agizo la Mhakama Kuu la Agosti 4,2025 lillotolewa na Jaji Hussein Mtembwa lililobainisha kuwa mashahidi ambao ni raia lazima walindwe kwa kuficha utambulisho wao wakati wale ambao si raia watatoa ushahidi kwa utaratibu wa kawaida.

Baada ya amri hiyo kutolewa maafisa wa Mahakama Kuu waliokuwa wakirusha mubashara kesi hiyo walilazimika kuzima kamera zao zote.Lissu anakabiliwa na kesi za uhaini ambayo inadaiwa Aprili 3,2025 jijini Dar es salaam alitoa kauli zinazodaiwa kushawishi umma kuzuia kufanya kwa ucahaguzi Mkuu wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments