Header Ads Widget

TANZANIA USO KWA USO NA MOROCCO KWA MKAPA


Tanzania dhidi ya Morocco Agosti 22,2025 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam katika hatua ya robo fainali ya mashinadano ya CHAN 2024 baada ya mechi za kundi A kumalizika huku Kenya ikiweka rekodi nzuri.

Morocco amabyo imemaliza nafasi ya pili kundi A, italazimika kusafiri mpaka Tanznia kwa ajili ya kukabiliana na Taifa Stars ya Tanzania ambayo ilifudhu hatua hiyo kabla ya kuisha kwa mechi za mwisho baada ya kushinda mechi tatu mfululizo.

Inakadiliwa kuwa mchezo kati ya Morocco na Tanznia utakuwa mchezo wa aina yake,,katika kundi lao Morocco imeshinda mechi tatu na kufungwa mechi moja wakati Tanznia imeshinda mechi tatu mfululizo na kutoa sare mechi moja na Taifa stars ya Tanzania kushika nafasi ya kwanza katika kundi B, huku Morocco ikishika nafasi ya pili katika kundi B,ikiwa ilipoteza mechi moja baada ya kuchapwa na Kenya.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kukutana na Morocco katika michuano ya CHAN 2024,Moroccoa imetwaa mara mbili ubingwa wa CHAN huku Tanznia ikitinga hatua hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara tatu michuano hii.

Post a Comment

0 Comments