Header Ads Widget

NGAO YA JAMII KUMKOSA SOWAH SEMPTEMBA 16



Mshambuliaji mpya wa Simba, Sowah ataikosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayopigwa Semptemba 16,2025 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa,Dar es salaam.

Hii ni baadaya ya kufungiwa kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho la CRDB msimu uliopita wakati akiwa na Singida Black Starts.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara,mchezaji anapopata kadi nyekundu katika michezo ya FA anatakiwa kutumikia adhabu hiyo kwenye mechi zinazofuata za mashindano ya ndani,ikiwemo ligi Kuu Bara,na pia Ngao ya Jamii.

Hii inamaanisha kwamba Sowah hataruhusiwa kushiriki mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya.Sowah alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha hili la kiangazi akitokea Singida Black Stars,na amukuwa akihesabiwa kama moja ya silaha mpya za kikosi cha kocha wa Simba Fadlu Davids


 

Post a Comment

0 Comments