TFF imetangaza kuwa mchezo wa Ngao ya Jamii kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2025/2026 utapigwa Semptemba 16,2025 jijini Dar es salaam.
Katika taarifa iliyotolewa na TFF imesema mchezo huo utawahusisha watani wa jaji Simba na Yanga ambapo Yanga alikuwa mshindi wa kwanza katika msimu uliopita huku Simba akiwa nafasi ya pili.
TFF imeongeza kwa kusema mfumo wa mashindano hayo ya ngao ya jamii umebadilika kutoka kucheza timu nne mpaka timu mbili kutokana na mabadiliko ya kanuni hivyo hautahusisha timu nne kama msimu wa nyuma utahusisha timu mbili.
Mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika kutokana na marekebisho ya kanuni yaliyopitishwa katika kikao kilichopita cha kamati ya Utendaji ya TFF.
Moja ya marekebisha yaliyofanyika ni katika hiyo ambapo ikitokea mazingira kama ya sasa ambapo mashindano ya Shirikisho la la Mpira wa miguu Africa (CAF) yamebana ratiba za TFF itachezwa mechi moja ya Ngao ya Jamii badala ya tatu ambapo huanzia na nusu fainali mbili na kumaliza na fainali.
.jpg)
0 Comments