Header Ads Widget

NYUMBA YA MCHUNGAJI YATEKETEA KWA MOTO TABORA


Mkoani Tabora moto wazuka na kuteketeza nyumba ya mchungaji wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora iliyopo barabara ya kilimatinde kata ya Cheyo manispaa ya Tabora.

Kwenye ajari hiyo ya moto iliyotokea usiku wa kumkia jana, hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini mali mbalimbali zilizokuwemo zimeteketea vibaya sna.

Mchungaji Amosi Chidemi ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo amesema saa moja usiku wakati akiwa sebuleni na familia yake wakaona moshi unajaa ndani na baad ya kwenda kuangalia unapotokea moshi wakaona moto tayari umeshatanda katika baadhi ya vyumba.

Amesema yeye pamoja na familia yake wametoka salama lakini hajui nini ambacho kimeokolewa mpaka kwani majirani walianza uokoaji wakati tayari moto umeshakuwa mkubwa 



 

Post a Comment

0 Comments