Uimara wa uliza wa Taifa stars katika mchezo wake wa leo dhidi ya Morocco kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa,Taifa stars itaikabiri Morocco ikiwa ni miongoni mwa timu zenye muendelezo mzuri na takwimu bora zaidi katika safu ya ulinzi katika mashindano hayo ambayo yatafikia tamati Agosti 30.
Hadi inafikia robo fainali Taifa stars imeruhusu gori moja tu na kabla ya mechi za jana za kundi D,ni timu tano tu ambazo zilikuwa zimefungwa bao moja moja ambazo ni stars,kenya,mauritania,sudan na senegal
Kitendo cha kuruhusu bao moja katika mechi nne kinaifanya Satrs iongoze katka chati ya timu zenye wastani wa kufungwa idadi ndogo ya mabao kwa mechi ambapo yenyewe,kenya na mauritania kila moja ina wastani wa kufungwa bao .03 kwa mchezo zikifuatiwa na sudan , algeria na senegal ambazo kila moja ina wastani wa kuruhusu bao 0.5.
Wakati stars ikiwa na takwimu bora za ulinzi kwenye michuano hii,Morocco yenyewe inayumbishwa na safu yake ya ulinzi kwani imeruhusu nyavu zake kutoborewa mara tatu katika mechi nne za mashindano hayo huku ikiwa na wastani mbovu wa kuruhusu bao.
.jpg)
0 Comments