Header Ads Widget

SIMBA YAPAA NAFASI MBILI YA KLABU BORA AFRICA.


Simba imeendelea kuonesha ukubwa wake Afrika baada ya kupaa katika viwango vya ubora wa klabu vya CAF hadi nafasi ya tano huku mtani wake Yanga naye akipanda kwa nafasi moja.

Kwa Simba kuwa nafasi ya tano inamaanisha imepanda kwa nafasi mbili kutokea nafasi ya saba ambayo ilikuwepo kabla ya kuanza msimu uliopita.Kwa mujibu ya chati ya CAF iliyotolewa leo,Simba ipo nafasi ya tano kutokana na pointi zake 48 ilizokusanya katika ushiriki wake kwenye mashindano ya klabu ya shirikisho hilo katika misimu mitano iliyopita

Wakati Simba ikiwa na pointi 48,Yanga ipo nafasi ya 12 kutokana na pointi zake 34 ambazo imezikusanya katika kipindi hicho.Kuwepo nafasi ya 12 kunamaanisha Yanga imesogea kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 13 ambayo ilikuwepo katika chati ya mwaka jana.

Chati hiyo ya CAF ndio itatumika katika kuchezesha droo ya mashindano ya klabu Afrika kwa msimu ujao ambayo imepangwa kufanyika kesho Jumamosi, Agosti 9,2025 Jijini Dar es salaam,Tanzania

Katika misimu mitano iliyopita Simba imefika hatua ya fainali mara moja na huku mara nne ikiishia robo fainali.Yanga ndani ya kipindi hicho imefika fainali mara moja na robo fainali mara moja na hatua ya makundi mara moja.


 

Post a Comment

0 Comments