Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la TAG darajani lenye urefu wa wa mita 0 na upana wa mita 7 linalounganisha jiji la Mbeya na wilaya ya Mbarali lilipo kata ya Nzagala jijini humo,limekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kuwa limerahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji
Akizungumza katika mahojiano maalumu,fundi sanifu mkuu TARURA wilaya ya Mbeya , Bw. Mayungu Mbita amesema kuwa wamepokea fedha shilingi milioni 299 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo baada ya daraja la awali kukatika na mvua
Wananchi wa maeneo wanajishughulisha na kilimo cha mbogamboga,mahindi na maharage,kujengwa kwa daraja hili kumerahisisha shughuli za kilimo cha kata hii na hata usafirishaji wa mazao baada ya mavuno.
Bw. Alfred Maneno mkazi wa kata hiyo ameongoza kwa kusema awali mvua zilikuwa zikinyesha daraja linakatika na kutupa ugumu wa usafirishaji wa mazao,pia ameongeza kwa kusema inatupa taaruki na mazingira hatarishi kwa kuwa hakukuwa na mawasiliano mazuri ililazimu kuzunguka kwenda barabara ya lami upande wa pili ili kufika mtaa wa Ndundu
.jpg)
0 Comments