Mahakama Kuu nchini Tanzania imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu walindwe.
Ina maana ya kwamba ushahidi wao utatolewa kwa kificho na hata utambulisho wao binafsi hautajulikana mfano majina yao halisi,familia zao na watu wakaribu yao kutojulikana,kutokana na taarifa ya gazeti la mtandaoni la Mwananchi Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa na Jaji Hussein Mtembwa jana Agosti 4,2025,kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP),imezuia pia taarifa zao kusambazwa,kuchapishwa na kutangazwa na chombo chochote cha habari,bila ridhaa ya mahakama.
Mwenyekiti huyo alikamatwa Aprili 9,2025 akiwa kwenye mkutano wa CHADEMA huko Mbinga kusini mwa Tanzania kisha kusafirishwa hadi Dar es salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10,2025
Lissu alikamatwa kwa kosa la kufanya chochozi wa kutofanyika uchaguzi mkuu 2025,baada ya kumaliza mkutano wa hadhara alipokuwa akiendelea kunadi msimamo wa chama hicho wa ''No Reforms,No Election, ikimaanisha bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Pia Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini ambalo halina dhamana kisheria na adhabu kwa mshtakiwa anayekutwa na hatia hiyo ni kifo.
.jpg)
0 Comments