Luhaga Mpina amefungua maisha mapya ya kisiasa ndani ya upinzani
Mbunge wa zamani wa Kisesa, mkoani Simiyu,Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea uraisi wa chama hicho.
Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema,mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya uraisi jana Jumatatu,Agosti 4,2025
Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa,baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa Ubunge wa Kisesa,kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo,Agosti 5,2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi,kamati kuu na halmashauri kuu,kuelekea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano,Agosti 6,2025.
Picha mbalimbali zimemuonesha Mpina akiwa anasajiliwa na Kiongozi wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu akimsajili kwa njia ya kidigitali
Kwa mujibu wa chanzo hicho,huenda kada huyo mpya akatambulishwa kwenye kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

0 Comments