Chama cha Mapinduzi (CCM) wameanza kutangaza matokeo ya kura za maoni za wagombea wa ubunge katika majimbo mbalimbali nchini,ambayo ni hatua muhimu kuelekea Uchaguzi mkuu Oktoba,2025
Kondoa Vijijini,Mjini
Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Kondoa Vijini,Dkt. Ashatu Kijaji ameongoza kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo,akiwashinda wenzake wanne.
Akitangaza matokeo hayo,Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa,Abdulrahim Hamidu amesema Dk Kijaji amepata kura 5,669 akifuatiwa na Hassan Lubuva aliyepata kura 3,593
Katika jimbo la Kondoa mjini,mariamu Ditopile ameongoza kura za maoni akipata kura 1869 akimshinda mbunge aliyemaliza muda wake,Ally Makoa amepata kula 843
Jimbo la Mpwapwa George Malima ametetea nafasi yake akipata kura 2665,Njamasi Chiwanga amepata kura 2140
Katika jimbo la Kibamba
Mshauri wa Rais,Angellah Kairuki ameibuka mshindi katika kura za maoni za ubunge za chama cha mapinduzi akipata kura za maoni 4655,akitangaza matokeo hayo katibu wa CCM wilaya ya ubungo, Henry Mwenge amesema Kairuki ameshinda kwa kupata kura 4655 huku akimbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Issa Mtemvu aliyepata kura 615
Aliye kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Dk Juma Homera ameongoza kura za maoni kwa kupata kula 11836 sawa na asilimia 92,akitrangaza matokeo hayo kaimu katibu wa wilaya Saidi Kusilawe.
.jpg)
0 Comments