Aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga ametetea nafasi yake baaday ya kuongoza katika kura za maoni za kuwania ubunge w Jimbo la Ludewa mkoani Njombe,Kamonga ametangazwa mshindi jana usiku Agost 4,2025 baada ya kupata kura 4099
Akizungumza na Upreality Tanzania leo Agosti 5,2025 msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa,Afred Mwambeleko amewataja wagombea wengine na kura zao kuwa ni pamoja na Philipo Filikunjombe,Merioni Ndofi James mkinga,Neema mturo,Zephania Chaula, na Anumie Mtwevi aliyeambulia kura 40.
Aliye kuwa mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA), Kunti Majala ameongoza kwenye kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Chemba.
Aliyekuwa mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa ameibuka kidedea katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi akipata kura 7902 na kuwaacha mbali wapinzani wake watano
Patrobasi Katambi amgalagaza Steven Masele mbali sana kura za maoni na Katambi kuibuka mshindi kwa ajiri ya kuipepelesha bendela ya Chama cha mapinduzi Oktoba 2025 katika Jimbo la Shinyanga Mjini.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda,ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa kupata kura 9056,kwa kula hizo Makonda anapewa dhamana ya kuipeperusha bendela ya CCM Arusha.
.jpg)
0 Comments