Header Ads Widget

POLEPOLE KUVULIWA HADHI YA UBALOZI

 


Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania ilitangaza rasmi kwamba aliyekuwa Balozi wa Tanzania Nchini Cuba,Polepole amevuliwa rasmi hadhi ya ubalozi kufuatia kwa uteuzi na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tangazo hilo lilihitimisha sura muhimu katika maisha ya mwanasiasa huyo,ambaye siku chache kabla alikuwa tayari ametuma barua ya kujiuzulu kwa kile alichokieleza kuwa kufifia kwa maadili ya uongozi wa kitaifa.

Polepole alipanda kwa kasi inayopingana na jina lake,Akiwa katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, sauti yake ilikuwa na uzito serikalini.Kisha akawa mbunge wa kuteuliwa,nafasi iliyompatia jukwaa la kuchambua,kushauri na wakati mwingine kuonyesha msimamo binafsi unaogusa mipaka ya ridhaa ya chama.

Baadaye alichaguliwa kuwa balozi japo hakuwekwa wazi katika uteuzi huo na haikuonesha anaenda nchi gani,uteuzi huo ulitosha kumuweka juu sana, kimuundo,kidiplomasia na kijamii.Alikuwa sehemu ya mfumo wa kimataifa wa uwakilishi wa Tanzania.Hatimaye,akatumikia kama Balozi nchini Malawi,kisha Cuba.Lakini Agosti 2025,hadhi hiyo inafika tamati ambayo kama alivyo wahi kusema mwandishi Pascal Mayalla, huja na heshima, kinga na nafasi ya kipekee, lakini si mali ya kudumu

Post a Comment

0 Comments