Kupitia msingi imara wa Diplomasia ya Kiuchumi na juhudi za kulinda amani na utulivu nchini, Mkoa wa Kigoma umeendelea kunufaika na miradi mikubwa ya maendeleo chini ya mpango wa TACTIC unaosimamiwa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa miradi hiyo ni:
Shilingi Bilioni 9.2: Ujenzi na ukarabati wa masoko ya Mwanga na Katonga.
Shilingi Bilioni 3.2: Upanuzi wa barabara ya Wafipa–Kagera na ujenzi wa daraja la Mto Luiche.
Shilingi Bilioni 8.6: Ujenzi wa barabara ya Bangwe–Ujiji yenye urefu wa Km 7.5.
Shilingi Bilioni 7.5: Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu Km 6.5 kwa kiwango cha lami.
Shilingi Bilioni 5.6: Ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji katika mitaa ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole, Bushabani, Mjimwema na Katonyanga.
Hii ni sehemu tu ya “mambo 10 muhimu” ambayo wananchi wa Kigoma wamenufaika nayo kupitia uongozi wa Dkt. Samia.
Kwa imani yao thabiti, wananchi hao wamemhakikishia Rais na wagombea wa CCM mapokezi makubwa kuelekea Oktoba 29, wakitarajia zaidi katika miradi ijayo kama vile:
Ukamilishaji wa ukarabati wa meli ya MV Liemba na ujenzi wa cherezo.
Ujenzi wa barabara ya Mpanda–Kigoma.
Kuimarishwa kwa shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika.
Kupanuka kwa biashara na ushirikiano wa kikanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na nchi jirani.
Kwa hakika, Kigoma inashuhudia mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii, matunda ya dira ya maendeleo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

0 Comments