Mpina aliwasili akiwa ameambatana na mgombea mwenza wake Fatma Ferej, huku akipokelewa na viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo Kiongozi wa Chama Dorothy Semu, Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo Omar Shaaban, mgombea ubunge wa Temeke Sheikh Ponda Issa Ponda, na Naibu Katibu wa Uenezi Taifa Shangwe Ayo.
Kurejeshwa kwa fomu hizo kunafuatia uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma uliotolewa Septemba 11, 2025, ambapo majaji walibatilisha zuio lililomnyima nafasi awali, wakibainisha kuwa mchakato uliotumika haukuwa halali kisheria. Uamuzi huo ulimfungulia njia Mpina kuendelea na mchakato kama wagombea wengine.
Kwa hatua hiyo, Mpina sasa anakuwa miongoni mwa wagombea urais watakaowania nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

0 Comments