Header Ads Widget

Real Madrid Yaivunja Barcelona Katika El Clásico ya Kusisimua Bernabeu

 


MADRID, Hispania — Katika pambano la kukata na shoka la Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga), maarufu kama El Clásico, lililochezwa Jumapili, Oktoba 26, 2025, klabu ya Real Madrid ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa jadi FC Barcelona, kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid. Ushindi huo umehitimisha rekodi mbaya ya Madrid ya kupoteza mara nne mfululizo dhidi ya wapinzani wao hao msimu uliopita, na hivyo kufufua hadhi yao mbele ya mashabiki.


Mchezo ulianza kwa kasi, ukidhihirisha ubora wa kiufundi na mbinu kutoka pande zote. Madrid walifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 22 kupitia kwa Kylian Mbappé, aliyemalizia kwa ustadi pasi murua kutoka kwa kiungo wa Kiingereza Jude Bellingham. Hata hivyo, Fermin Lopez aliisawazishia Barcelona dakika ya 38 akipokea pasi safi kutoka Marcus Rashford. Dakika chache kabla ya mapumziko, Bellingham aliipatia Madrid bao la pili katika dakika ya 43 baada ya krosi ya kichwa kutoka Eder Militao, na kuufanya Uwanja wa Bernabeu kulipuka kwa shangwe.


Kipindi cha pili kilijaa presha na mbinu za hali ya juu, huku Barcelona wakijaribu kurejea mchezoni licha ya kuwakosa wachezaji muhimu. Madrid ilidhibiti mchezo kwa nidhamu na ubora mkubwa hadi filimbi ya mwisho. Dakika za nyongeza zilimgeukia Pedri wa Barcelona kuwa na bahati mbaya baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano, na hivyo kutolewa nje, jambo litakalomfanya kukosa mechi ijayo dhidi ya Elche mnamo Novemba 2, 2025.


Ushindi huo umeipa Real Madrid nafasi ya kuendelea kileleni mwa msimamo wa LaLiga ikiwa na pointi 27, ikitangulia Barcelona wenye pointi 22.

Mchezo huo pia ulikumbwa na idadi kubwa ya wachezaji waliokosekana kutokana na majeraha:

Barcelona: Robert Lewandowski, Raphinha, Dan Olmo, Gavi, kipa Marc-André ter Stegen, na mabeki Andreas Christensen pamoja na Joan Garcia. Kocha Hans Frick naye alikosa mchezo kutokana na adhabu ya kadi nyekundu.


Real Madrid: Antonio Rüdiger na David Alaba waliendelea kuwa nje kutokana na majeraha.



Kwa ujumla, ushindi huo wa mabao 2-1 umeimarisha nafasi ya Real Madrid katika mbio za ubingwa na kuvunja "laana" ya vipigo kutoka Barcelona, tukio lililowapa mashabiki wao furaha kubwa baada ya muda mrefu wa kusubiri.

Post a Comment

0 Comments