Watu 25 wafariki Dunia katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la shule lililowabeba waombolezaji katika eneo la mamboleo Coptic ,kaunti ya Kisumu,nchini Kenya.Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii nchini Kenya,ajali hiyo imetokea Agosti 8,2025 ikielezwa uchunguzi kwa awali umebaini dereva alipoteza udhibiti wa basi hilo kwenye barabara ambayo ajali hutokea mara kawa mara.
Imeelezwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba waombolezaji kutoka kwenye mazishi Kusini Magharibi mwa Kenya lilipinduka hadi kwenye Mtario na kusababisha vifo vya watu 25.Dereva alishindwa kulidhibiti basi hilo lilipokaribia mzunguko wa barabarani likiwa katika mwendo kasi,hivyo likatumbukia kwenye mtaro.
Kwa mujibu wa Peter Maina ofisa wa uasalama wa barabarani katika mkoa wa Nyanza Gari lilipoteza udhibiti likapinduka na kubilingilitia mtaroni upande wa pili wa barabra.
Fredrick Olunga katibu mkuu anayesimamia huduma za matibabu nchini Kenya amesema watu 21 walifariki dunia eneo la tukio huku watu 4 walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitalini.
.jpg)
0 Comments