Header Ads Widget

KESI DHIDI YA CHADEMA KUAMULIWA AGOSTI 18,2025


Mahakama Kuu masijala ndogo Dar es salaam, Agosti  18,2025 imepanga kutoa uamuzi kuhusu shauri la maombi ya marejeo ya Chadema ya kupinga amri za Mahakama hiyo,kuizuia kwa muda kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali zake.

Uamuzi huo utatolewa baada ya Alhamisi Agosti 7 cham hicho kuwasilisha hoja zake mahakamani kikilenga kuishawishi ikiondolee amri hizo.Mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Jaji Hamidu Mwanga wa Juni 10,2025 ilikizuia kwa muda chama ch Democrasia na Maendeleo kufanya shughuli za kiasiasa na kutumia mali zake mpaka kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali inayokikabili itakapoamuliwa.

Uamuzi huo ulitokana na maombi yaliyowasilishwa na walalamikaji katika kesi ya kikatiba na kusikilizwa kwa upande baada ya aliyekuwa wakili wa Chadema, Jebra Kambole kujiondoa kwenye kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka  2025 imefunguliwa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema, Saidi Issa Mohamed na wajumbe wawili wa bodi ya wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar,Ahmed Rashid Khamis na Maulid Anna Komu.

Wadaiwa ni Bodi ya wadhamini wa Chadema na katibu Mkuu wa Chama hicho.Walio fungua shauri hilo wanadai kumekuwa na mawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Zanzibar na Tanzania Bara kinyume cha sheria ya vyama vya siasa na katiba ya chama hicho.
 

Post a Comment

0 Comments