Header Ads Widget

SAMIA RASMI KUCHUKUA FOMU YA URAIS INEC KESHO


Chama cha Mapinduzi CCM  kimesema Rais Samia Suluhu Hassan,ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho atachukua rasmi fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM kesho Jumamosi,Agosti 9,2025 saa 4;50 asubuhi katika ofisi ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (inec) jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 8,2025 Katibu wa itikadi na Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla,amesema Rais Samia ataambatana na mgombea mwenza wake Dk. Emmanuel Nchimbi katika hafla hiyo ya kuchukua fomu katika Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).

Makalla ameongeza kuwa Rais Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama chetu ndiye mgombea wa Chama Cha Mapinduzi.Baada ya kuchukua fomu atarejea kwenye ofisi ya chama Dodoma na atapata fursa ya kusalimiana na wana CCM ambao tumewakaribisha katika katika tukio hilo.


 

Post a Comment

0 Comments