Header Ads Widget

MPINA,OTHUMAN WAPOKELEWA KWA KISHINDO UNGUJA


Umati wa wananchi na wanachama wa ACT wazalendo mjini Unguja wamefurika kuwapokea watiania wa urais wa Hamhuri ya Muungano Tanzania,Luhaga Mpina na Othuman Masoud wa Zanzibar waliokwenda kujitambulisha.

Wananchi na wanachama hao walianza kujitokeza eneo la Bandari ya Malindi ambako Mpina,Othuma na Fatuma Abdulhabibi Ferej Mgombea mwenza walitua mjini hapa leo Jumamosi Agosti 9,2025 wakitokea  Dar es salaam.

Watiania hao wamesindikizwa na kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu makamu mwenyekiti wa chama Isihaka Mchinjita na Ismail JUma Mkamu mwenyekiti,Katibu Mkuu Ado Shaibu na wajumbe wa kamati kuu ya chama.



 

Post a Comment

0 Comments