Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imekumbusha wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mwaka wa masomo ujao kuwa wana siku tisa pekee kumaliza maombi yao ya mikopo.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa waombaji kuhakikisha wanafanya uhakiki wa taarifa zao,kupakia nyaraka sahihi,na kukamilisha usajili wao kabla ya tarehe ya mwisho.
Kwa mujibu wa HESLB, mfumo wa maombi unapatikana mtandaoni saa 24 na unarahisisha wanafunzi wa ndani na nje ya nchi kujaza taarifa zao bila usumbufu. Aidha imeelezwa kuwa kuchelewa au kuwasilisha maombi yenye mapungufu kunaweza kusababisha kuondolewa kwenye orodha ya waliokubaliwa kuapata mikopo.
Serikali imesisiza dhamira yake kusaidia vijana kufanikisha ndoto zao za kielimu kupitia mikopo,huku ikitoa wito kwa wazazi na walezi kushirikiana kwa karibu na watoto wao katika hatua za maombi.

0 Comments