Chama Cha Mapinduzi kimeanza rasmi mchatao wa ndani wa kuwateua wagombea watakaoshiriki katika uchaguzi mkuu ujao.Hatua hii ni sehemu ya taratibu za chama katika kuhakikisha kwamba wagombea wanaopitisha wanakidhi vigezo vya uongozi na kukubarika na jamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi wa Chama hicho mchato utahusisha hatua kadhaa zikiwemo,wajumbe kuchambua wasifu wa waombaji nafasi mbalimbali,kamati za siasa ngazi ya wilaya,mikoa na taifa kushiriki kutoa mapendekezo,Uhakiki wa maadili,uadilifu wa kijamii kabla ya kuidhinishwa rasmi.
CCM imesisitiza kuwa uteuzi wa wagombea hautaegemea maslai binafsi bali maslai ya taifa na uhalisia wa uongozi unaoweza kutekelza ilani ya chama
Aidha, viongozi wa chama wamewahimiza wanachama wote kushiriki kwa amani na mshikamno,wakieleza kwama umoja wa ndani ya chama ndio msingi wa ushindi kwenye uchaguzi.

0 Comments