Header Ads Widget

KAULI ZA POLEPOLE ZAZUA MAJIBU KUTOKA INEC NA NIDA


Baada ya aliyekuwa katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, Polepole,kutoka maoni kuhusu mwenendo wa taasisi za uchaguzi na uasajili wa wanancnhi mashirika husika yameibuka kutoka ufafanuzi.

Polepole alinukuliwa akisema kuwa mchakato wa uchaguzi na utambulisho wa wananchiu bado una changamoto zinazoweza kuathiri haki ya kidemokrasia.kauli hizo zimepelekea Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kujibu hoja kwa kueleza hatua zinachukuliwa kuboresha mifumo yao.

Kwa Upande wa INEC maofisa wamesema maandalizi ya uchaguzi ujao yanaendelea kwa uwazi na ushirikishwaji wa wadau wote,huku wakiahidi kutumia tecknolojia kuongeza uaminifu wa matokeo.

NIDA nayo imesisitiza kuwa kazi ya kusajili wananchi inaendelea kwa kasi,na tayari imeimarisha mifumo ya kidigitali ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata kitambulisho cha Taifa kwa wakati.

Kauli hizi zinaibua mjadala mpya juu ya nafasi ya taasisi huru katika kuhakikisha uchaguzi wa kidemokrasia na ushiriki wa wananchi bila vikwazovya kiutawala.

Post a Comment

0 Comments