Katika hatua mpya zilizojitokeza leo,Mahakama Kuu imesikiliza hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa uteuzi wa wagombea uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi.Upande wa walalamikaji umedai kuwa taratibu fulani za ndani ya chama hazikufuatwa ipasavyo,jambo lililopelekea mgogoro huu kufikishwa mahakamani.
Wakili anayewakilisha upande wa walalamikaji alisisitiza umuhimu wa uwazi na usawa katika kchakato wa kugombe nafasi ya juu ya uongozi wa Taifa,akieleza kuwa ni haki ya kila mwanachama kuoata nafasi ya kushiriki bila upendeleo.
Kwa upande wake mawakili wa CCM wameeleza kuwa mchakato uliofuata katiba na kanuni za chama na kwamaba madai yaliyowasilishwa hayana msingi wa kisheria.wameiomba mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa inalenga kudhoofisha uhalali wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu.
Mahakama imetangaza kuwa itaendelea kusikiliza ushahidi na hoja za pande zote kabla ya kutoa uamuzi.Hali hii imezua mjadala mpana katika jamii kuhusu naman vyama vya siasa vinavyoshughulikia demokrasia ya ndani na nafasi ya mahakama katika kulinda haki za kisiasa.

0 Comments