Header Ads Widget

BOCCO NA MKUDE KUAGWA KWA HESHIMA YA KIPEKEE SIMBA DAY

Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa itatumia mkutano wake mkubwa wa kila mwaka,Simba day ,kuaga rasmi wachezaji wake wazoefu na waliotumikia timu kwa muda mrefu-John Bocco na Jonas Mkude.

Bocco na Mkude wamekuwa nguzo muhimu ya Simba kwa miaka mingi,wakichangia mafanikio makubwa ya kikosi hicho,ikiwemo makombe ya ligi kuu Bara,michuano ya FA na kushiriki mara kwa mara kwenye michuano ya kimataifa ya CAF.

Katika taarifa yake, ungozi wa Simba umesema tukio hilo litakuwa ni njia ya kuwashukuru wachezajihao kwa mchango wao mkubwa ndani ya timu na pia kuwapa nafasi mashabiki kuwaaga kwa heshima kubwa.

Bocco na Mkude si wachezaji wa kawaida. Ni sehemu ya historia ya Simba na mchango wao hautasaulika.Simba day ya mwaka huu itakuwa maalumu kwao,imeeleza klabu kupitia taarifa yake.

Wapenzi wa Simba SC na mashabiki wa soka nchini wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo ambalo litapambwa na burudani mbalimbali na mechi ya kirafiki ya kimataifa.


 

Post a Comment

0 Comments