Mwanasiasa machachari na mbunge wa zamani wa Mbulu Vijijini,Flatei Massay,maarufu kama ''Mzee wa sarakasi Bungeni''aibukia rasmi chama cha upinzani ACT-Wazalendo baadaya ya jina lake kufyekwa katika mchakato wa uteuzi wa wabunge watakao ipeperusha bendera ya CCM.
Massay aliwahi kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na ucheshi,mbwembwe na sarakasi zake bungeni,jambo lililompa heshima na kutambulika si tu kama mbunge wa kawaida bali kama kioo cha mijadala yenye mvuto bungeni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kujiunga na ACT,Massay alisema,Kutoswa na CCM si mwisho wa safari yangu ya kisiasa.Nitaendeleza kusimsmia na wananchi kupitia ACT-Wazalendo,chama kinachoamini katiak uwazi na usawa.
Uongozi wa ACT ulimkaribisha rasmi, wakisema ujio wake ni ishara ya upanuzi wa wigo wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Wachambuzi wa siasa wanasema hatua ya Massay inaweza kuibua mvuto mpya wa kisiasa katika maeneo ya kanda ya kaskazini,ambako amewahi kushika nafasi kubwa ya ushawishi
.jpg)
 
 
 
 
 
 
 
0 Comments