Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024) yamehitimisha safari ya wenyeji baada ya kuondolewa mapema,jambo lililowaacha mashabiki wakiwa na hisia mchanganyiko.Hata hivyo,timu ya wenyeji imepongezwa kwa nidhamu,kiwango kizuri cha uchezaji na maandalizi mazuri yaliyovutia mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuaga mashindano mapema,wenyeji wameacha alama kubwa kwa kujanza uwanja na kuvunja rekodi mbalimbali,Tanzania pekee imeshiriki mara tatu na mara mbili wameishia makundi na mara moja wametinga mpaka robo fainali ambapo kwa wachambuzi wanasema hiyo ni hatua nzuri sana kwa Taifa Stars,
Huku Kenya wakishiriki mara ya kwanza na kutinga robo fainali,hivyo Kenya wameandika historia ya kufika robo fainali ya michuano hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki.
Uganda kama wenyeji wa michuano hiyo ambapo imeshiriki mara nyingi zaidi bila mafanikio yeyote amabyo ni chanya, awamu hii Uganga imetoa gundu kwa kufika rbo fainali ya michuano ya CHAN 2024 kwa mara ya kwanza tokea ianze kushiriki michuano hii.
Lakini upeo wa matumaini sasa unahamia mwaka 2027,pale ambapo Kenya,Uganda na Tanzania kwa pamoja wataandaa AFCON 2027 kwa mara ya kwanza katika historia ya ukanda wa Afrika mashariki.Hii inatazamwa kama fursa ya kipekee ya kuinua kiwango cha soka,kukuza miundombinu ya michezo na kuonesha uwezo wa kanda hiyo kuandaa michuano mikubwa ya timu 36 ambapo ukanda huu upewa jukumu la kuandaa michuano hii na kuweka maandalizi ya viwanja 12,Tanzania imepewa jukumu ya kuwa na viwanja vyenye ubora wa kimataifa 4,huku Kenya imepewa jukumu la kuandaa viwanja vyenye ubora wa kimataifa 5 na Uganda viwanja 3.
Mashabiki na wenyeji wa CHAN 2024 ni kielelezo kwamba soka la Ukanda wa CECAFA hii itakuwa ni mara ya pili kuletwa ukanda huu ikiwa mara ya kwanza waliandaa Ethiopia.Hii inaonesha ustawi mzuri wa soka la Africa mashariki na kwamba mashindano yajayo ya AFCON 2027 yatakuwa kipimo kikubwa cha mafanikio hayo.
.jpg)
0 Comments