Chama Cha Mapinduzi kimepata sura mpya katika safu ya uongozi wake baada ya kumtangaza Dk. Asha-Rose Migiro kama Katibu Mkuu mpya wa chama hicho.
Tangazo hili limefanywa na vikao vya juu vya chama leo,hatua ambayo imepokelewa kwa hisia mbalimbali kutoka kwa wananchi na wanachama wa siasa nchini.
Historia fupi ya Dk. Migiro
Dk. Migiro ni mwanasiasa na mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa,aliyewahi kushikilia nafasi ya:
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)
Uzoefu huu unatajwa kama moja ya sababu kubwa zilizompa nafasi ya kuongoza idara ya utendaji wa CCM.
Maana kwa CCM
Uteuzi wa Dk. Migiro unaangalia kama mkakati wa chama kuimarisha uongozi wake kuelekea uchaguzi mkuu,huku akitarajiwa kuleta mabadiliko katika usimamizi wa sera,mawasiliano na maandalizi ya kisiasa ya chama hicho tawala.
Kauli za mwanzao
Akizungumza mara baada ya uteuzi wake Dk. Migiro amewashukuru wajumbe wa CCM kwa imani waliyoonesha kwake,akiahidi kushiriakiana na viongozi na wanachama wote katika kusukuma mbele ajenda ya chama na maendeleo ya Taifa.
.jpg)
0 Comments