Katika mchakato wa ndani wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kumetokea jambo la kushangaza ambapo wajumbe watano kati ya 19 wa zamani wa CHADEMA wamefanikiwa kupenya na kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM.
Hali hii imeibua mijadala mitandaoni na ndani ya vikao vya siasa,ikichukuliwa kama ushahidi wa CCM kuendelea kuvutia makada kutoka vyama vya upinzania nchini Tanzania.
Majina ya waliopenya kwenye Ngome hizo ni:
Esther Matiko -Tarime Mjini
Ester Bulaya -Bunda Mjini
Hawa Mwaifunga -Tabora Mjini
Kunti Majala -Chemba
Jesca Kishoa -Iramba Mashariki
Mantiki ya Uteuzi
Kwa wachambuzi wa siasa, hatua hii inatazamwa kama mkakati wa CCM kuimarisha nafasi zake kwa kuchukua makada waliowahi kushinda kwenye maeneo yenye ushindani mkubwa,huku pia ikionesha ulegevu wa upinzania katika kudumisha wanachama wake waandamizi.
Muktadha
Kwa ujumla,mchakato wa uteuzi wa CCM mwaka huu umeacha gumzo kubwa kutokana na majina makubwa kuanguka na sura mpya kupenya, hatua ambayo wengi wanaiona kama mwendelezo wa siasa za ushindani ndani ya chama hicho tawala.

0 Comments