Kocha mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge ameibua gumzo baada ya kufanya maamuzi mazito ya kuwatema baadhi ya nyota waliokuwa tegemeo ndani ya kikosi hicho.Hatua hiyo imeibua maswali mengi miongozni mwa mashabiki wa soka lakini ukweli ni kwamba Ibenge ana sababu madhubuti ambazo zinaonesha mwelekeo mpya wa Azam FC msimu huu.
NIDHAMU NA MAADILI YA KIFUNDI
Ripoti toka benchi la ufundi zinaonesha kuwa baadhi ya wachezaji walikuwa wakihusishwa na changamoto za nidhamu,jambo ambalo limekuwa likimkera Ibenge,kocha huyo anaamini nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio ya timu yoyote na bila hilo hata vipaji vikubwa havina tija.
MKAKATI WA KIKOSI KIPYA
Anataka kuijenga Azam yenye mwelekeo mpya,ikijikita kwenye wachezaji wachanga wenye ari na uwezo wa kupambana kwa dakika 90.Mastaa wengine waliokatwa walionekana kushindwa kuendana na kasi ya mfumo huo mpya.
MCHANGO UWANJANI
Wapo wachezaji waliokuwa wakipata nafasi nyingi lakini mchango wao ulikuwa mdogo,ameweka wazi kwamba nafasi ya kucheza Azam itatolewa kwa wale wanaothibitisha thamani yao uwanjani si majina pekee.
MAANDALIZI YA MASHINDANO MAKUBWA
Klabu ikpo kwenye maandalizi ya ligi Kuu Bara pia inataka kufanya vizuri kimataifa,ameona ni muhimu kuwa na kikosi chembamba chenye ubora badala ya kutegemea wachezaji wenye majina makubwa wasiotoa matokeo.
UWEKEZAJI WA KLABU
Klabu imeamua kuwekeza kwa wachezaji wapya na vijana waliokuja kwa gharama nafuu lakini wenye uwezo mkubwa wa kuapanda chati.Hatua hii inalenga kuifanya Azam kuwa klabu endelevu bila kutegemea mastaa wa muda mfupi.
Ameongeza kwa kusema kwa sasa mashabiki wa Azam wanatakiwa kujiandaa kuona timu yenye sura mpya na Ibenge anaamini maamuzi haya magumu ndiyo yatakayojenga msingi wa mafanikio ya muda mrefu.
.jpg)
0 Comments