Header Ads Widget

MPASUKO ACT-WAZALENDO:MPINA AONDOLEWA KWENYE UWANJA WA URAIS


Taarifa za hivi punde kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania zinaonyesha kuwa uteuzi wa Luhaga Mpina kama mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo umesitishwa rasmi.Hatua hii ilichukuliwa kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Monalisa Joseph Ndala,katibu Mwenezi wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es salaam,ambaye alidai kuna ukiukwaji wa taratibu za chama katika uteuzi huo.

Mpina alijiunga na ACT tarehe 5 Agosti,2025 na kupitishwa rasmikuwa mgombea uraisi tarehe 7 Agosti 2025,alishtakiwa kutokidhi masharti yaliyofafanuliwa kaatika sheria ya Chama miongoni mwa hayo ni lazima mgombea awe mwanachama kwa siku 7 kala ya uteuzi hata siku 30 kama ilivyo katika kanuni za zamani.

Baada ya mbio ya katiba,Msajili alikutana na wanasiasa hao Agosti 23,2025 kabla ya kutoa uamuzi huu rasmi wa kuuteketeza uteuzi wake mpaka chombo chake kiwe kinatambua taratibu zote za chama zimezingatiwa.

 

Post a Comment

0 Comments