Header Ads Widget

DK MIGIRO AKABIDHIWA OFISI: TUPO TAYARI KUKITETEA CHAMA


Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi,Dk Asha-Rose Migiro,amekabidhiwa rasmi ofisi yake Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma na kutoa kauli nzito ya mshikamano akisema chama kiko imara na kiko tayari kukitetea katika kila hatua.

Hafla ya makabidhiano hayo ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo wajumbe wa kamati Kuu,Wabunge, na Makatibu wa wilaya,ambapo ilitawaliwa na shangwe na matumaini mapya ya safari ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi Dk Migiro alisema,CCM imejengwa kwa misingi ya umoja na mshikamno. Hatujaja kubadilisha msingi,bali kuimarisha misingi hiyo kwa nguvu mpya.Tupo tayari kukitetea chama na kuhakikisha kinaendelea kuongoza taifa letu kwa uadilifu na mshikamano.

Aidha aliwaimiza vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na maendeleo,akisisitiza kwamba CCM ni chama cha watu wote na hakina mgawanyiko.

Viongozi walioshiriki hafla hiyo walisema wa Migiro ni ishara ya mabadiliko chsnya na uthibitisho wa nafasi ya wanawake katika siasa za Tanzania.

Kwa upande mwingine wachambuzi wakisiasa wameona tukio hilo kama sehemu ya maandalizi ya chama kuelekea chaguzi zijazo huku wakitabiri ongezeko la ushindani wa hoja ndani ya siasa za nyama vingi nchini.

 

Post a Comment

0 Comments