Header Ads Widget

INEC: WAGOMBEA URAIS,UBUNGE NA UDIWANI TANZANIA KUJULIKANA LEO


Dodoma -  Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) leo Agosti 27,2025 kuanzia majira ya saa 1:30 hadi majira ya saa 10:00 jioni, inatarajiwa kutangaza rasmi majina ya wagombea watakaopitishwa kuwania nafasi za urais,ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Taarifa kutoka makao makuu ya tume hiyo zinaeleza kuwa mchakato wa uhakika na uchambuzi wa fomu za uteuzi umekamilika,na leo wanachi watapata orodha kamili ya wagombea watakaoshiriki katika kinyang'anyiro hicho.

Kwa mujibu wa ratiba ya tume,matangazo hayo yatafanyika jijini Dodoma na kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni mbalimbali na mitandao mbalimbali ya kijamii, ili kuhakikisha wananchi wote wanapata taarifa kwa uwazi.

Wadadisi wa siasa wanasema tukio hili ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi,kwani litaweka wazi mizani ya kisiasa na mikakati ya vyama mbalimbali.Wengine wanasubiri kwa hamu kuona kama je jina la anaetarajiwa kuwa mpizani mkubwa wa chama tawala Luhaga Mpina tume itataja jina lake licha ya msajili wa vyama vya kisiasa kutengua uteuzi wake wa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo.

INEC imewaakikishia wananchi kuwa mchakato wote umezingatia misingi ya uwazi,haki na usawa, huku ikiahidi kushughulikia changamoto zote zinazoweza kujitokeza.



 

Post a Comment

0 Comments