Header Ads Widget

INEC YAMWENGUA LUHAGA MPINA KUWANIA URAIS TANZANIA


Safari ya kisiasa ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya ACT,Luhaga Mpina imekumbwa na pigo kubwa baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumwengua rasmi katika kinyang'nyiro hicho ch urais wa Tanzania 2025.

Taarifa za INEC iliyotolewa leo imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baaday ya kupitia kwa kina nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa na kubaini kasoro kadhaa zilizomnyima siafa za kuendelea na mchakato wa kugombea.

Uamuzi huu unakuja siku chache baada ya mvutano ulioibuka ndani ya ACT,ambapo Katibu wa Itikadi, Uenezi ma Mawasiliano wa Chama,Monalisa Ndala aliwasilisha malalamiko kwa Msajili wa vyama vya siasa akipinga uhalali wa Mpina kupitishwa kama mgombea urais.

Kwa mujibu wa INEC, miongoni mwa sababu zilizotajwa ni kutokidhi baadhi ya masharti ya kikatiba na kisheria ya kugombea nafasi ya juu ya uongozi nchini,jambo ambalo lililofanya jina la Mpina kutupiliwa mbali kwenye orodha ya wagombea wa urais.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema tukio hili linaweza kuathiri mshikamano wa ACT-Wazalendo kuelekea uchaguzi mkuu,kwani linakuja kipindi ambacho chama hicho kilihitaji kuimarisha mshikamano wa ndani na kujipanga kukabiliana na vyama vikuu.

Kwa sasa macho ya Watanzania yanaelekezwa kwa ACT kuona ni nani atakayeibuliwa kama mgombea mpaya wa urais, au chama hicho kitatafuta suluhu ya haraka ili kuokoa taswira yake kisisa kabla ya uchaguzi.

 

Post a Comment

0 Comments