Header Ads Widget

RAIS SAMIA AONGOZA NJIA:INEC YATHIBITISHA UTEUZI WAKE


Katika hatua iliyoteka macho ya wengi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,amekuwa mgombe wa kwanza kuthibitishwa rasmi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania urais wa mwaka 2025 kupitia CCM.

Tukio hili limeibua hisia tofauti katika duru za kisiasa,ambapo wachambuzi wanaliita kama ishara ya uthabiti wa CCM na pia mkakati wa chama kuhakikisha wanatangulia katika mbio za kisiasa kabla ya vyama vingine kukamilisha taratibu zao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na INEC, Rais Samia alikidhi masharti yote ya kisheria na kikatiba,ikiwa ni pamoja na kukusanya idadi ya kutosha ya wadhamini kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.Uamuzi huu unamweka mbele ya wagombea wengine ambao bado wanapita mchakato wa uhakiki.

Hadi sasa mbali na CCM,vyama vingine vilivyokwishawasilisha majina ya wagombea ni:
AAFP -Kunje Ngombare Mwiru
NRA - Hassan Almasi
Chama cha Makini - Coaster Kibonde
NLD - Doyo Hassan Doyo
UPDP - Twalibu Kadege

Hata hivyo,wagombea hawa bado hawajathibitishwa rasmi kama ilivyo kwa Rais Samia.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema hatua hii inaipa CCM nafasi ya kujiamini na kuonyesha umakini katika maandalizi yao.Aidha,hatua ya Rais Samia kutangulia imeonekana kama ushindi wa kisaikolojia dhidi ya wapinzani,hasa wakati ambapo vyama vingine vinapambana ndani kujua nani atawakilisha chama chao.

INEC imetangaza kuwa orodha ya mwisho ya wagombea wa urais,ubunge na udiwani itatolewa muda mfupi baada ya taratibu za uhakiki kukamilika. Kwa sasa,macho yote yanamwangalia Rais Samia kama kiongozi aliyepiga hatua ya mwanzo kwa ujasiri katika uchaguzi wa mwaka huu


 

Post a Comment

0 Comments