Chama cha ACT kimefungua shauri la maombi kuhusiana na uteuzi wa mgombea wake wa nafasi ya Urais,Luhaga Mpina,baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ku mzuia kurejesha fomu yake ya kuomba uteuzi aliyokabidhiwa awali kuijaza.
Chama hicho kimefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu,Dodoma,Leo Jumatano Agosti 27,2025,kikiomba mahama hiyo iilekeze INEC ipokee fomu ya mgombea wao huyo kwa ajili ya uhakiki na uteuzi.
Mwanasheria mkuu wa ACT, Omar Issa Shaaban,ameeleza leo kuwa kuwa shauri hilo lililopewa usajili wa namba 21692 la mwaka 2025 limefunguliwa leo chini ya hati ya dharura sana,na limepangwa kusikilizwa kesho Alhamisi,Agosti 28,2025.
Shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya wadhamini waliosajiliwa wa ACT na Luhaga Mpina,dhidi ya INEC na mwanasheria mkuu wa serikali.
.jpg)
0 Comments