Kama ulikuwa unazani ni ndoto mbaya za Man U zimeisha,subiri kidogo,Jana usiku mashabiki walishuhudia kile kinachoitwa ''Fedheha'' ya mwaka baada ya Red Devils kulimwa na timu ndogo ya daraja la nne Grimsby Town kwenye Kombe la Carabao.
Katika dakika za mwanzo,mambo yalionekana kama mzaha.Charles Vernam aliifungia Grimsby bao la kwanza dakika ya 22,na Tyrell akazidisha aibu kwa bao la pili dakika ya 30 baada ya kipa Onana kufanya kosa la kizembe.Mashabiki wa Grisby wakapagawa,wengine wakaanza kuimba kwisheni kazi United''
United wakajitutumua dakika ya 75 kupitia Bryan Mbeumo,kabla ya nahodha wa ''fedheha'' Maguire kusawazisha dakika ya 89 kwa kichwa cha kufa mtu. Hapo mashabiki wa United wakapata matumaini ya dakika za majeruhi kumbe ilikuwa ndoto ya mchana.
Mchezo ukaenda moja kwa moja penati na ndipo drama ikaanza.mashabiki walishuhudia penati nyingi kupigwa na kufungwa mapaka kufikia 12-11 na unajua nani aliharibu? Bryan Mbeumo akapiga penati ya mwisho mpira ukagonga mwamba
Mashabiki wa United wakabaki mdomo wazi wengine wakabandika tagi mpya ''Red devels wamekuwa red tears.mitandaoni mashabiki wa Grimsby walicheka hadi kusema ''Tulikuja kwa mabasi na tumerudi na Historia
.jpg)
0 Comments