Dar es Salaam: Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Tanzania (dcea) imethibitisha kufanikisha hatua kubwa ya matibabu kwa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Chid Benz.Hatua hii imempokelewa kw faraja kubwa na mashabiki,wadau wa sanaa na familia yake,ikionesha mabadiliko makubwa katiaka mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Kwa muda mrefu, Chid Benz alihusishwa na changamoto za uraibu wa dawa, jambo lililodhoofisha maendeleo yake ya muziki na maisha binafsi. hata hivyo kupitia mpango maalumu wa matibabu na ushauri nasaha ulioendeshwa na DCEA msanii huyo sasa anaendelea vizuri na ameonyesha mabadiliko chanya.
Kamishina wa DCEA amesema kuwa mafanikio ya Chid Benz ni ushahidi wa dhahiri kwamba matibabu na msaada wa kitaalamu vinaweza kumrejesha kijana yeyote kwenye maisha yenye tija.
Kwa upande wa Chid Benz amewashukuru mashabiki wake na DCEA kwa kutomtelekeza,Nimepata nafasi ya pili maishani. Muziki wangu utakuwa chombo cha kutoa elimu na kutia moyo vijana kuepuka dawa za kulevya
.jpeg)
0 Comments