Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es salaam,leo Alhamisi, Agosti 7 2025 inatarajia kusikiliza shauri la maombi ya marejeo lililofunguliwa na Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kupinga amri za kukizuia kufanya shughuli za siasa na kutumia mali zake.
Amri hizo za zuio dhidi ya chama zilitolewa na Jaki Hamidu Mwanga Juni 10,2025,kufuatia sharti la maombi lililofunguliwa na walalamikaji katika kesi ya madai dhidi yake kuhusu mgawanyiko wa rasilimali kati ya Bara na Zanzibar.
Kesi hiyo namba 8323 ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, makamu mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA,Zanzibar na wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa CHADEMA kutoka Zanzibar,Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Walalamikiwa ni Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama hicho
Sambamba na kesi hiyo pia walalamikiwa hao walifungua shauri dogo la maombi ya zuio la muda dhidi ya wadaiwa,wakiomba Mahakama itoe amri ya kuwazuia kufanya shughuli zozote za kisiasa na kutumia mali za chama mpaka kesi hiyo ya msingi itakapoamuliwa.
Awali,walalamikiwa walipambana kuimaliza kesi hiyo kwa mbinu za kiufundi baada ya kuwasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya msingi na dhidi ya shauri dogo la maoni ya zuio lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kwani Juni 10,2025 mahakama hiyo iliyatupilia mbali
Vilevile, ilisikiliza shauri la maombi ya zuio ambayo katika uamuzi wake ilikubaliana na hoja za walalamikaji na kukizua chama hicho shughuli zote za kisiasa,Hivyo Mahakani mbali na amri ya zuio kwa walalamikiwa kushughulisha na shughuli zozote za kisiasa,pia iliwazia waadawa hao binafsi,wakala wao au mtu yeyote anayefanya kazi kwa maelezo au kwa niaba yao,kutumia mali za chama hicho mpaka kesi ya msingi itakapo amuliwa.
Walalamikiwa hawakukubaliana na uamuzi huo,hivyo wakafungua shauri la mrejeo,wakiiomba Mhakama irejee na kisha iondoe amri hizo wakidai zilitolewa isivyo halali.
Sambamba na shauri hilo la mrejeo pia waliandika barua ya kumkataa Jaji Mwanga wakimtaka ajiondoe kusikiliza kesi hiyo wakidai kuwa hawana imani naye.Jaji Mwanga baada ya kusikiliza sababu zao za kumkataa katika uamuzi wake alioutoa Julai 28,2025,alikisema hoja zao hazikuwa na msingi wa kisheria.Aliamua kuwa ataendelea kusikiliza kesi hiyo na akapanga kusikiliza shauri lao la marejeo leo Agosti 7,2025.Hivyo wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo,mawakili wa CHADEMA watakuwa na kibarua kizito kuishawishi mahakama kuwa ilikosea katika kutoa amri hizo na hatimaye iziondoe.
.jpg)
0 Comments