Header Ads Widget

SALUM MWALIMU APEWA RIDHAA YA KUIPEPERUSHA BENDERA YA CHAUMMA 2025


Naibu Katibu wa Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA, Benson Kigaila amemtangaza katibu Mkuu wa chama hicho,Salum Mwalimu atakuwa mpeperusha Bendera wa chama hicho kwenye mbio za uchaguzi Oktoba 29,2025.

Kigaila amemtangaza kiongozi huyo kwenye mkutano mkuu wa Chaumma unaoendelea Mlimani city leo Alhamisi Agosti 7,2025.

Kigaila amesema jina la Kiongozi huyo lilipendekezwa na Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama yenye jukumu la kuleta mapendekezo ya jina la mgombea urais Tanzania na Zanzibar katika kikao kilichofanyika jana.

Baada ya kufanya utafifiti na kufikiri kwa kina ni mtu gani anaweza kutuvusha,Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuja na jina la Salumu Mwalimu,anatufaa kutuvusha kwenye mbio za uraisi wa Tanzania,amesema Kigaila.

Kulingana na maelezo ya Kigaila amesema mchakato wa kumpata Salum waliopita hadi kufika kupata, kwanza walifanya utafiti na katika utafiti huu,Tuliangalia nani anaweza kutufaa na kutuvusha,tulifanya mazingatio tukimteuua mtu anajua matatizo ya watanzania akiona anaweza kuumizwa na kuyashughulkikia.

 

Post a Comment

0 Comments