Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imezindua kampeni y elimu ya kodi kwa biashara yya mtandaoni kwa lengo la kuhakikisha kila anayehusika na biashara hizo anajisajili ili aanze kulipa kodi
Akizindua kampeni hiyo jijini Dar es salaam kamishina Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema wanaolenwa katika usajili huo ni wafanyabiashara wenye kipato cha zaidi ya sh. milioni 4 kwa mwaka ambao kodi yao itakuwa shi. 100.000 kwa mwaka na kila mmoja atalipa kulingana na kipato chake.
Mwenda amesema wakati wakiendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wote wanaofanya biashara za mitandaoni kujisajili wataanza na wanaofanya biashara ya kukodisha nyumba mtandaoni na wale wanaoenesha biashara mtao ambao wamekuwa wakipata fedha nyingi na hawalipi kodi.
Amesema TRA itatoa asilimia tatu 3% ya kodi itakayookolewa kwa watu wataotoa taarifa za ukwepaji wa kodi kwa wafanyabiashara watakaoshindwa kujisajili ndani ya muda uliowekwa na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wanaokwepa kodi na watawatambua kwa kutokutoa risiti.

0 Comments