Header Ads Widget

WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI SHINYANGA WAFUKIWA NA KIFUSI


Wachimbaji 25 katika mgodi mdogo wa dhahabu unaomilikiwa na kikundi cha Wachapakazi,uliopo kijiji cha Mwongozo,kata ya Mwenge,Halimashauri ya Shinyanga  mkoani Shinyanga,wamefukiwa na kifusi baada ya mgodi huo kutitia wakati zoezi la ukarabati wa madauara likiendelea.

Tukio hilo limetokea majira ya asubuhi,ambapo watu hao walikuwa wakifanya matengenezo kwenye mashimo matatu tofauti,duara namba 106 lilikuwa na wachimbaji 6,duara namba 103 wachimabji 11 na duara namba 20 wachimaji 8.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya shinyanga ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Mtatiro,inaendelea na zoezi la uokozi kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na Uokoaji pamoja na wachimbaji wenzao.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni kutitia kwa ardhi wakati shughuli ya matengenezo ya mduara ikiendelea 

Hadi sasa zoezi la uokoaji limefanikiwa kwa kuokolewawatu watatu kati 25 waliofukiwa kwenye mgodi huo.jitihada za kuwaokoa wengine zinaendelea chini ya usimamizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji.

Post a Comment

0 Comments