Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto (unicef),wameendeleza juhudi kubwa za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi Wilayani Uyui,Mkoani Tabora,ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuinua ubora wa elimu nchini.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano maalumu yaliyosainiwa kati ya TEA na UNICEF, yenye lengo la kuboresha miundombinu ya elimu katika mikoa ya Tabora,Kigoma na Songwe.kupitia ushirikiano huo,jumla ya miradi 48 ya elimu inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.
Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui,miradi minne tayari imekamilika ikiwa na thamani ya takribani shilingi milioni 162.8. miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika shule ya Sekondari Nsololo,pamoja na ukarabati na umalizaji wa maabara nne za masomo ya sayansi katika shule za sekondari za Goweko,usagari na kizengi.
Utekelezaji wa miradi hiyo umekuwa chachu ya maboresho makubwa katika mazingira ya kujifunzia na hivyo kuchochea ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi mmoja mmoja pamoja na maendeleo ya kitaalamu katika shule kwa ujumla.
Mkuu wa ya swkondari Nsololo mwalimu Pulina Mareko alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huo,shule ilikuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya vyoo.
0 Comments