Header Ads Widget

UGONJWA ULIOONDOA UHAI WA NDUGAI SPIKA MSTAAFU WA BUNGE LA TANZANIA


Wakati Katibu wa Bunge la Jamuhuri la Muungano Tanzania Baraka Leonard akisema Spika mstaafu amefariki danuania kwa shinikizo la damu kushuka lililosababishwa na maambukizi makali kwenye mfumo wa hewa,wataalamu wa afya wameuelezea ugonjwa huo.

Leo Agosti 10,2025 wataalamu wa afya wamesema shinikizo la damu kushuka ni hali inayotokeza wakati shinikizo la damu linapo kuwa chini ya kiwango kusukuma damu kufika sehemu muhimu za mwili.

Wamesema hali hiyo husababisha ogani muhimu za mwili ikiwamo ubongo,moyo na figo kukosa hewa ya kutosha hivyo huweza kusababisha kifo.Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospital ya taifa ya muhimbili ELisha Osati amesema mtu anapopata maambukizi makali ya bakteria au virusi au fangasi huweza kumletea septic shock hali inayosababisha presha ya damu yake kupungua.

 

Post a Comment

0 Comments